Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Abu Ubaidah Msemaji wa kundi la Jihad Al-Islam akieleza kupinga baadhi ya madai ya Jumuiya za Kimataifa kusema kua Jihad Al-Islam katika vita ya siku nane na Israel walitenda unyama dhidi ya Wananchi wa Israel, Ila maneno hayo yalipingwa vukali na msemaji huyo wa Jihad Al-Islam akisema: Sisi hatuna silaha za kisasa ambazo twaweza kuzitumia dhidi ya Wananchi wa Israel na ulimwengu wafahamu hilo.
Akiendelea kusema: Wapiganaji wa Jihad Al-Islam na Opresheni zao dhidi ya jeshi la Israel ni kupiga kambi za kijeshi na si kupiga makazi ya Wananchi kama wanavyofanya wao, Na madai ya Jumuiya za Kimataifa ni uongo na maneno hayana uhakika ndani yake.
Katika kila vita au mashambulizi ya Israel dhidi ya Palestina Jumuiya ya Kutetea Haki za Binadamu ilikilaani vikali unyama unaofanywa na majeshi ya Mazayuni (Israel) dhidi ya Wapalestina.